kujifunza biblia pamoja

[A short note to those readers who do not speak (or read) Swahili:  I’ve decided to begin publishing on the blog some of my Swahili Bible study materials.  I realize many of you who have subscribed to aliens and strangers may not be interested in receiving posts you cannot read by email or blog reader.  I want to ask, though, that you consider keeping your subscription and skipping over the few posts that are written in Swahili (it will indeed be only a few posts).  My intention is not to begin writing a lot of blog posts in Swahili.  Rather, I’ve noticed there are East Africans who occasionally read the blog, and I thought some of the Bible study materials I’m teaching might be helpful to someone out there.  Also, I’ve not located a great deal of information in Swahili on the subjects of Church Planting Movements (CPM) or Discovery Bible Studies (DBS).]

 


Nakusudi kuitambulisha njia ya kujifunza Biblia pamoja.  Kwanza, lakini, bora nifafanue kwa kifupi maana ya kusisitiza utaratibu wa vikundi badala ya kumtegemea mwalimu mmoja tu.

  • Kwenye Biblia, mara nyingi twaona mifano ya Mungu kutumia vikundi.  Analenga vikundi wa watu wanaofanya kazi pamoja.  Aliteua taifa moja liwe la kwake — Wayahudi — lina koo 12.  Yesu aliwateua na kuwatuma watu 12. Pia, aliwachagua na kutuma 70 (Luka 10), wawili na wawili.  Baada ya Yesu kufa na kufufuka, alianzisha kanisa lake, lililo kikundi cha watu washirikianao kwa makusudi yake.  Mungu anatumia vikundi.
  • Haiwezekani mtu mmoja kuwa mfuasi mkweli wa Yesu peke yake.  Ni lazima ashirikiane, kusaidiana, na kutegemeana na wafuasi wengine.
  • Ni bora hatumtegemei kiongozi mmoja wa kutuhamasisha, kutulisha, na kutukomaza kwenye neno la Mungu.  Agano Jipya haitaji watu wa Mungu kumtumainia mtu mmoja wa kutuongoza sote — isipokuwa Yesu Kristo, kichwa chetu.  Wote wengine ni viungo vya mwili wake.  Na kazi yetu ni, kwa pamoja, kumwakilisha Mungu duniani.  Kila mkristo ni kiungo tu, na sisi wote tunacho kichwa moja — Yesu Kristo.
  • Watu wengi pale wanaposhirikiana wana akili zaidi ya mtu mmoja peke yake.
  • Watu wengi wajifunza haraka kuliko mtu mmoja peke yake.
  • Si mara nyingi kwamba kikundi cha watu wajifunzao Biblia kwa pamoja na kurekebishana kukosa kwenye maelewano yao (kwa muda mrefu).  Wakristo ambao wamefuata uzushi ni wakristo ambao wategemeao watu wengine kufikiri kwa niaba yao.  Na wapokea kila neno wanalosema bila ya kujifunza wao wenyewe.  [Lazima tuyachunguze Biblia kila siku ili tujue kama wanachosema wengine (viongozi, wamisionari, n.k.) ni kweli.  Tuufuate mfano wa Waberea kwenye Matendo 17:10-11.]

Hivyo, ni lazima utaratibu wetu wa kujifunza Biblia uwawezeshe wote washirikiane na kusaidiana.  Tusimtegemee mtu mmoja kutulisha sote chakula cha kiroho.  Kama sisi ni mwili wa Yesu, inatubidi tufanye kazi kwa pamoja ili tukomae kwa pamoja.

Wajibu wa viongozi wa kanisa sio kuwakomaza watu wa Mungu; huu ni wajibu wa Mungu mwenyewe kupitia Roho Mtakatifu aishiye ndani yetu.  Wajibu wa viongozi vya kanisa ni kuwaandaa watu wa Mungu wamsikilize na kumtii Mungu kwa njia ya kushirikiana na kusaidiana na Wakristo wa kanisa lao.

Tutafute njia ya kujifunza Biblia inayotuwezesha kusaidiana na kushirikiana zaidi, badala kuwategemea viongozi tu.  Wiki ijayo, nitatoa ratiba ya “Maongezi ya Biblia.”


* Hii ni mara yangu ya kwanza kutumia Kiswahili katika blog yangu.  Kusema wazi, mpaka sasa nimeogopa  wengine hawataelewa vizuri ninachoandika.  Naomba mnisaidie, lakini, kuendeleza Kiswahili changu; nisahihishe kama nimekosea.

Advertisements

1 Comment

Filed under kiswahili

One response to “kujifunza biblia pamoja

  1. moses kipchumba sambu

    good swahili lesson.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s